UPDATES: Sentensi 2 za Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni Akimtumbua RTO Pwani


Naibu waziri wa Mambo ya Ndani amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani.

Mhandisi Hamad Masauni amesema “RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutaki uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania,”

“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria.”  alisema Masauni

0 Comments:

Post a Comment