Arusha Vicoba Empowerment Ltd imeendesha Mafunzo Maalum kwa Vikundi vya kiujasiriamali .

Mh. Emanuel Kessy Diwani wa kata ya Kaloleni (Katikati) ambaye ni mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo , wengine ni Kulia Bi. Grace Macha Mkurugenzi wa Arusha Vicoba Empowerment Ltd. , Mwenyekiti wa Arusha Vicoba Empowerment Ltd, pamoja na Afisa kutoka Meru Community Bank Bw. Honest Mungure na Afisa Maendeleo kata ya Levolosi Bi. Joyce Kimbute

Arusha Vicoba Empowerment imeendesha Mafunzo hayo mapema leo huku lengo ikiwa kuboresha uendeshaji na ukuaji wa Vikundi vya Saccoss kwa ajili ya kujikuza kiujasiriamali na hatimaye lufikia malengo tarajiwa.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya Vicoba alikuwa Diwani wa kata ya Kaloleni Mh. Emanuel Messy

Akihutubu katika hafla hiyo Mh. Kessy amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Kujiunga katika vikundi vya kiujasiriamali ili kurahisisha kupata mikopo kutoka serikalini  au kwenye taasisi zingine.

Pamoja na kuipongeza Kampuni ya Vicoba ya Arusha Vicoba Empowerment Ltd kwa kujilita katika kuleta mabadiliko kwenye shughuli za maendeleo hasa kuinua kipato cha wananchi kupitia Vicoba na kutoa Mafunzo mbalimbali ili kukumbushana majukumu na wajibu wa vikundi vya kiujasiriamali.

Mwenyekiti wa Arusha Vicoba Empowerment Ltd Bw. Hassan Moses Amejikita katika kuwaelimisha wanavikundi kujikumbusha kufahamishana majukumu ya kila mmoja katika vikundi kuanzia majukumu ya vuliongozi kwa nafasi zao.

0 Comments:

Post a Comment