UPDATES: Taratibu za Mazishi ya mwili wa Mzee wetu Ndesamburo

Msiba mkubwa wa chama (CHADEMA) wa Mzee Ndesamburo ,
Mazishi ya Mh Philemon Ndesamburo yatafanyika siku ya Jumanne 6/6/2017 nyumbani kwake Mtaa wa KDC, Kata ya Kiborloni Manispaa ya Moshi.
Hii ni kwa mujibu wa

Pia kabla ya mazishi kutatanguliwa na siku ya kumbukizi ambayo itakua siku ya Jumatatu katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sindato Ndesamburo Kiwelu, ambae ni msemaji wa familia amesema siku hiyo ya Jumatatu mwili wa marehe utatolewa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC asubuhi na kupelekwa moja kwa moja katika viwanja hivyo vya mashujaa.

Amesema kuwa wananchi watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwa siku nzima, na pia viongozi mbalimbali watahutubu na kumweleze mh Ndesamburo katika Historia yake kwa jinsi walivyomjua katika maisha yake.

Aidha amesema kuwa mwili wa marehemu utaondolewa viwanjani hapo majira ya saa kumi jioni siku hiyo na kupelekwa nyumbani kwake ambapo taratibu nyingine zitafuata.

0 Comments:

Post a Comment