Kamanda mmoja mwandamizi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab amejisalimisha kwa jeshi la taifa la Somalia.
Kamanda mkuu wa jeshi la Somalia, Jenerali Ahmed Mohamed Tredishe amesema mwanachama huyo wa al-Shabaab anayejulikana kwa jina Bishar Mumin Afrah amejisalimisha kwa jeshi hilo katika mji Buloburte eneo la Hiran, yapata kilomita 200 kaskazini mwa Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Inaarifiwa kuwa, kamanda huyo mwandamizi wa genge la kigaidi la al-Shabaab amejisalimisha kwa vyombo vya usalama sambamba na kukabidhi bunduki mbili aina ya AK47 na shehena ya risasi.
Hivi karibuni Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo alitoa msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo wa al-Shabaab ambao wataweka silaha chini na kujisalimisha kwa serikali.
Endelea kubaki nami ikiwa ni pamoja na kwenye Mitandao ya kijamii Facebook ,Twitter, Instagram, kote kwa jina la Habari Tanzania Grace Macha bila kusahau kutazama Latest Videos zote katika V.O.A TV YouTube

0 Comments:
Post a Comment