ADIMU: PICHA 2/ VIDEO Kakakuona aonekana Matejoo Arusha

Kakakuona ni mnyama ambaye huonekana kwa nadra sana ulimwenguni huku baadhi ya tamaduni huamini kuwa anapoonekana Ni Baraka juu ya jambo Fulani au jambo Fulani hutokea. Ni viashiria vya matukio yatatotokea katika jamii Fulani. 
  Zaidi hapo chini Ni maelezo yake.

Kakakuona ni wanyama wa familia ambao wamepambika na magamba na wana mkia mrefu. Wakitaka kujikinga dhidi ya wanyama hatari wanajikunja.
Huishi katika kishimo cha kina cha hadi mita 3.5 au katika mti mvungu.
Hula mchwa na sisimizi na pengine wadudu wengine ambao huwakamata kwa ulimi wao mrefu wa kunata. 
IPO HAPA VIDEO FUPI KUTOKA V.O.A TV IKIMUONEAHA KAKAKUONA HUYO

Huzaa kidogo sana, na hiyo imechangia kufanya wapungue sana. Sababu nyingine ni ushirikina unaodai wanaleta bahati njema, hasa magamba yao. Ndiyo sababu nchini Tanzania wanalindwa na sheria kali hata wasikamatwe.

0 Comments:

Post a Comment