MFUNGO WA RAMADHAN: Lowassa awatakia mfungo mwema waislam


"Jumamosi ya tarehe 27 mwezi huu,ndugu zetu waislam hapa nchini wanaungana na wenzao kote duniani, kuanza kutekeleza moja ya ibada zao muhimu,KUFUNGA RAMADHAN.


Ni kipindi ambacho Waislam wanatakiwa kutenda mema zaidi na kuwa karibu zaidi na mwenyezimungu kwani malipo katika mwezi huu ni mara dufu zaidi ya miezi mingine.


Nachukua nafasi hii kuwatakia ndugu zangu waislam mfungo mwema katika mwezi huo mtukufu wa Ramadhan, na kuwaomba wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula katika mwezi.Pia nawaomba  ndugu zetu wakristo na wa dini nyingine kuwa na ushirikiano na wenzao kama ilivyo desturi yetu, ili watimize ibada hii muhimu kwao.


Kwa wale wenye uwezo tuwasaidie wenzetu wasiyokuwa nao na pia katika ibada zetu tuiombee nchi yetu amani na utulivu  na pia kuomba hekima na busara zitawale ndani ya vichwa vya viongozi wetu."

Edward Lowassa(Waziri/Mkuu wa zamani)



0 Comments:

Post a Comment