HIVI PUNDE: Hawa ni viongozi waliotoa salamu za pole kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini Philemon Ndesamburo , "Nafuta Machozi nikimaliza nitaeleza Yale mengi ambayo umeyafanya nikishuhudia siyo kuhadidhiwa..."

Mh.Zitto Kabwe , Nh. Mbowe, na Bi. Grace Macha
Zitto Kabwe , Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe , na Mkurugenzi wa Arusha Vicoba Empowerment Bi. Grace Macha waungana na Chadema kumlilia shujaa mwanamageuzi Philemon Ndesamburo

Mwenyekiti Wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe 

Dodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema alipopata taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alijaribu kumzuia mtoto wa marehemu, Lucy Owenya asichangie bungeni  lakini alishindwa.

Mbowe ameyasema hayo leo Jumatano wakati akilitangazia bunge kuhusu kifo cha Mwenyekiti huyo wa Chadema, mkoa wa Kilimanjaro.

Owenya ni mbunge wa viti maalum wa chama hicho na mtoto wa kada huyo mkongwe wa Chadema.

 "Ilipofika zamu yake kuchangia nilimruka hata akalalamika inakuwaje wakati alitakiwa atoe maoni yake. Tushirikiane na familia ya marehemu ambaye alihudumu kwenye bunge hili kukamilisha taratibu zilizobaki," amesema Chenge.

Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ametuma salamu za rambi rambi kwa wanachama wa Chadema  baada ya kuondokewa na kiongozi wake mkubwa, Philemon Ndesamburo.

 Pia Zitto amempa pole, mtoto wa marehemu Ndesamburo, Lucy Owenya kwa kumpoteza baba yake.

Zitto ameandika katika ukurasa wake wa Facebook leo na kusema; “Ni msiba mkubwa kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa Pesa alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015. Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu kingine chochote.”

Zitto amesema msiba wa Ndesamburo ni mkubwa kwa wanaChadema ambacho alikuwa Mwenyekiti wake wa  Mkoa tangu chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta.

 “Huwezi kutaja maendeleo ya Chadema kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la mzee Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi kwa karibu, naweza kutamka bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda chama chake kwa dhati kabisa,” amesema

Kadhalika Zitto anaendelea kummwagia sifa Ndesamburo akisema Tanzania ina faidi matunda ya vyama vingi kwa sababu ya kazi kubwa aliyofanya Mzee Ndesamburo.

“Nawapa pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya Mzee Ndesamburo. Mzee wetu aliishi maisha yake na ameacha ' legacy ' yake. Najua maumivu yenu lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye mtihani huu mkubwa. muwe wamoja na mshikamane.” Amesema na kuongeza:

“Poleni sana ndugu zangu wa Chadema kwa kupotelewa na kiongozi wenu na kiongozi wetu pia.  Poleni sana wana Moshi Mjini na wana Kilimanjaro wote. Poleni Sana Watanzania.pumzika kwa Amani Philemon Kiwelu Ndesamburo. Hiyo ni njia yetu sote. Amina.”

Godbless Lema Mbunge Wa Arusha Mjini

" Mzee Ndesamburo alikuwa mtu Wa muhimu sana katika chama na kwa Taifa kwa ujumla, tunaungana na familia ya Marehemu"

Grace Macha Mkurugenzi Wa Arusha Vicoba Empowerment.

"Nafuta Machozi nikimaliza nitaeleza Yale mengi uliyoyafanya nikiyashuhudia kwa macho so ya kuhadidhiwa......"



0 Comments:

Post a Comment