Taarifa
inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati Kuu ya Chama, chini ya Mwenyekiti
wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika kikao chake cha kawaida kwa
mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika kikao
hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala
mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu
uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;
1. Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi
Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
2. Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu
za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda
dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
3. Taarifa za utendaji wa chama kupitia
kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
4. Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya
kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.
5. Taarifa za mwenendo wa shughuli ya
uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya
Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu.
Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015
na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara a Habari na Mawasiliano-
CHADEMA
0 Comments:
Post a Comment