FROM NKMB JJ MNYIKA ON BARAZA LA MAWAZIRI LA JK
Baraza bado ni dhaifu; Rais alipaswa kutumia mabadiliko haya kuondoa mawaziri wote ambao walisemwa na upinzani, wananchi na hata baadhi na CCM yenyewe kuwa ni mizigo.
Badala yake mabadiliko haya pamoja na kuziba mapengo ya Muhongo na Tibaijuka, yamelenga kupunguza majeraha ya mivutano ya ndani kwa ndani ndani ya Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais kutokana na makundi ya urais ya ndani ya CCM.
Wananchi wasitegemee mabadiliko makubwa kutokana na baraza hili na yasitumike kuwapa matumaini hewa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 badala yake nguvu zielekezwe kujiandikisha kupiga kura, kuiondoa CCM uchaguzi 2015 kuwezesha Baraza la Mawaziri la UKAWA kuteuliwa na kuongoza mabadiliko nchini.
Aidha, mabadiliko ya baraza hili hayatazuia haja ya Serikali kutoa taarifa Bungeni juu ya utekelezaji wa maazimio yote ya Bunge juu ya kashfa ya Escrow na hoja ya kutaka mchakato wa kura ya maoni usitishwe na maandalizi yaendelee kuwezesha uchaguzi ujao kuwa huru na haki na kuwezesha mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya nchi na wananchi. JJ Mnyika (MB).
Sent from Grace Macha
Watu 75 Wameokolewa, zoezi la uokoaji linaendelea kwa ufanisi
-
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Juhudi za Serikali kupitia vikosi mbalimbali katika zoezi la uokoaji wa
manusura wa ajali iliyotokea jana Novemba 16,2024...
1 hour ago
0 Comments:
Post a Comment