WAANDISHI WA HABARI WAZURU MLIMA KILIMANJARO


SAM_0064

Mhifadhi wa Utalii wa
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Eva Mallya akizungumza
 katika ziara ya waandishi wa habari kutoka Arusha walikwenda kutembelea
hifadhi hiyo na kujionea shughuli  mbalimbali za utalii ikiwemo
kivutio cha kupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima pekee mrefu na kilele chake kina
Barafu Barani Afrika.

SAM_0013Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa na mmoja wa wafanyakazi wa KINAPA mara baada ya kuwasili

 

SAM_0010

Baadhi ya sehemu ya waandishi wa habari

SAM_0058

 SAM_0066Muonekano ndani ya ukumbi wa mkutano katika makao makuu ya KINAPA

SAM_0074Mwandishi wa hazeti la Tanzania Daima Grace Macha akifanya mahojiano na RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65)ambaye  ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro

SAM_0054Mmiliki wa mtandao wa jamiiblog Pamela Molle wakiwa anasalimiana na mwandishi mwandamizi wa gazeti la The citizen  Patty Magubira

SAM_0076Mwandishi wa habari Leo Veronicah Mheta akipozi katika picha na RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65) ambaye ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro

SAM_0078

Mwandishi wa Uhuru Lilian Joel akiwaanafanya mahojiano na RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65) ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro

SAM_0086RAIA wa Nchini Japan ,ambaye ni mlemavu wa miguu na kupoza mwili upande wa kushoto Eiju Murakami (65) ambaye ametimiza ndoto yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa anaonyesha cheti chake mara baada ya kukabidhiwa pembeni ni muongoza watalii

KOMBE la Dunia linachangia baadhi ya watalii kushindwa kufika Nchini
Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro kutokana na watu mbalimbali kuwa
makini na mpira kuliko suala la utalii.
Hayo yalisemwa jana Mkoani Kilimanjaro na  Mhifadhi wa Utalii wa
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Eva Mallya wakati
alipokuwa akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali wanaotembelea
hifadhi hiyo kujionea shughuli za  mbalimbali za utalii ikiwemo
kivutio cha kupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima pekee wenye
Barafu Barani Afrika.
Alisema mashindano ya kombe la Dunia yanapofanyika baada ya miaka mine
kupita idadi ya watalii wanaotaka kutembelea vivutio vya utalii
inapungua kutokana na watalii hao kupenda kuangalia mpira zaidi.
Alisema ingawa mashindano hayo yanapofanyika yanaleta manufaa kwa kila
nchi lakini nchi nyingine zenye kutangaza masuala ya utalii idadi ya
wageni inashuka kutokana na wageni wengi kupendelea mpira zaidi.
Alisema hifadhi hiyo inawatalii wa mataifa mbalimbali wanaitembelea
kutokana na vivutio vilivyopo vya wanyama, mazingira pamoja na
upandaji wa Mlima Kilimanjaro ambao ni wa kipekee na wenye barafu.
Alisema mwaka  fedha 2011/12 idadi ya wageni kutoka nchi mbalimbali
iliongezeka na kufikia 57,456 ambayo ni kubwa zaidi lakini mwaka
2012/13 wageni walikuwa 55,553 huku mwaka 2013/14 walipungua na
kufikia  51,286.
Alisema sababu za kupungua kwa watalii wanaofika Kinapa mojawapo ni
mashindao ya kombe la Dunia, mtikisiko wa uchumi pamoja na ukosefu wa
ajira.
"Kombe la Dunia linachangia wageni kutofika kutembela vivutio vya
utalii ndio yanapofanyika mashindano yanafaida zake lakini pia
kunasababu mbalimbali ila kwakuwa Mlima Kilimanjaro unajiuza tunapata
wageni wa mataifa mbalimbali na pia nawaomba watalii wa ndani na wan
chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) watembelee hifadhi hii ya
Kinapa".

--
from Grace Macha
+255754283612

0 Comments:

Post a Comment