Kikwete kachoka kuwaongoza watanzania au ni ufisadi mwingine..

Kikwete ndo ameanza mapumziko yake baada ya "kuchoka na kazi ya
kuiongoza nchi"kabla ya kumaliza awamu yake October, 2015. Kama
mtakumbuka alikuwa US hivi karibuni kwa "ziara" ya wiki mbili. Habari
toka ubalozi wa Tanzania US zinadai kwamba Kikwete atakuwa US kuanzia
Alhamisi ya wiki hii (November 6th, 2014) kwa "ziara binafsi" ya siku
20. Atakuwa Baltimore na atafikia katika hotel ambayo atalipa $5,000
kwa siku na inasenekana atakuwa na kundi la watu 17. Hii itakuwa ni
ziara ya tatu ya Kikwete US katika kipindi cha miezi mitatu. Hii ni
gharama ya chumba cha hotel tu kwa mtu mmoja, bila kujumlisha gharama
za wengine na wala kuhesabu gharama za usafiri, chakula na mambo
mengine: $5000 X Tsh 1707 x siku 20 = Tsh. 170,700,000 X 17
=2,901,900,000 hakika huu nibufisadi mwingine anaufanya kikwete..

0 Comments:

Post a Comment