MWANAFUNZI KIDATO CHA 5 IHUNGO AJINYONGA HADI KUFA KWA KUNYIMWA HUDUMA YA MATIBABU ALIPOKUWA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA MJINI BUKOBA.
Mwanafunzi wa kidato cha 5 shule ya sekondari Ihungo mjini Bukoba kwa majina Ezra Gerald amejinyonga hadi kufa baada ya kukaa hospitalini kwa siku 3 bila kupewa matibabu yoyote.
Taarifa inariport kuwa alilazwa hospitalini toka 11/09/2014 hadi 15 bila kuhudumiwa.
Baada ya kutelekezwa na wauguzi na madaktari wa Hospitali hiyo aliamua kujiua kwa kujinyonga.
Aliandika maneno haya kwenye karatasi ya kauli yake ya mwisho kwa watakaoshuhudia mwili wake.
"Haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa. Nakaa hospital bila kuhudumiwa, badala yake kusodolewa na wauguzi".
Akaendelea,
"Siwezi kuendelea kuwa hospital bila matibabu ilhali wengine wanaendelea na masomo".
Chanzo: Matukio Radio Free Afrika (RFA). 18/09/2014
Maoni yangu:
Haya ni matokeo ya serikali dhalimu isiyokuwa na vipau mbele sahihi.
Ccm inapeleka mabilioni kwenye mbio za mwenge zisizokuwa na tija yoyote, bali kuharibu fedha za umma bila mrejesho kwa maisha ya Watz.
1. Uharibifu wa fedha/mabilion ya Watz ktk bunge fake la Katiba ya ki ccm bila haya wala bofu kwa Mungu.
Ajabu eti wanasali. Aibuuuu kwa ccm.
2.Ccm imepeleka mabilioni kwenye sherehe za Muungano,
3.ufisadi wa Escrow,
4.wizi halmashauri zote nchini,
5.udhaifu mkubwa wa kifisadi bandali zote nchini.
6.kumbuka wizi wa fedha za Epa zilizokwapuliwa na watu Kikwete alusema anawajuwa.
7. Majangiri wanaolindwa na serikali ya ccm, Kikwete alisema ana orodha ya majangiri papa 40 hadi leo hajawachukulia hatua.
Niishie hapo, maovu ni mengi sana siwezi kuyamaliza.
Ajabu hadi sasa hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.
Ufisasi huo ukifanyika majanga yanayowakuta akina Ezra, akina mama ktk hospitali za umma kote nchini yanasikitisha sana.
Hospital za umma hazina msaada bali mateso,
Mashuleni, mahakamani, barabarani, n.k kote ni majanga yanayotesa Watz.
Ujumbe:
Ukombozi ni lazima upatikane, na Katiba mpya iliyo bora ni lazima ipatikane na siyo ya ki-ccm bali ya Watz, na siyo hisani ya ccm bali ni haki ya Watz.
Tukifanikisha katiba mpya iloyo bora tutakombolewa na kupata amani na uhuru wa kweli.
Ezra ni mmoja wa Watz wanaokumbwa na masahibu ya kupoteza maisha kwa kifo kinachoweza kuzuilika.
Watz wazalendo tusikubali kuburuzwa na Chama cha magamba ccm.
Tujiandukishe kupiga kura, na tupige kura kwa viongozi bora wa upinzani siyo ccm.
Usikubali kuwa Ezra wa kesho, saidia kuokoa roho za Watz kwa kukataa ccm, na washirika wao wakandamizaji wa Watz hasa wanyonge.
Wafikishie Watz wengi ujumbe huu. Ili ukombozi tuutafite kwa ushirikiano.
Nguvu ya Umma inapokuhitaji kupitia sanduku la wapiga kura au vinginevyo usikose kushiriki.
Shiriki kuwakomboa akina Ezra waliohai wasijinyonge kama yeye, watoto, akina mama, wazee, n.k kwa kukataa udhalimu wa mafisadi wasiokuwa na huruma dhidi ya Watz.
Peoples Power!!
M4C Pamoja Daima.
Solomon Kambarangwe
18/09/2014
Sent from my iPhone
LLA inavyoweza kuleta afua katika athari ya mabadiliko ya tabianchi
-
Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Ingawa mabadiliko ya tabianchi yanatajwa kuuathiri ulimwengu
kwa ujumla wake, kiuhalisia Bara la Afrika ndilo linalojikuta k...
56 minutes ago
0 Comments:
Post a Comment