Baraza Kuu la Chadema lililoketi mwaka jana, pamoja na masuala
mengine, lilipitisha mabadiliko ya kanuni (ikiwa ni moja ya affairs
zake kikatiba), ambapo mojawapo ya masuala iliyoyatungia kanuni ni
pamoja na Kamati Kuu kushughulikia masuala ya dharura kwa niaba ya
Baraza Kuu na kuweka utaratibu/mfumo wa Kanda.
Sasa moja ya sifa nzuri za Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006 ni kwamba
inajumuisha mambo yafuatayo; Katiba yenyewe, kanuni za uendeshaji
chama, maadili na itifaki.
Sasa baada ya Baraza Kuu kufanya kazi yake ya kikatiba ya kutunga na
kuridhia kanuni, ilikuwa lazima ziingizwe ndani ya Katiba ya Mwaka
2006, ndiyo maana sasa ilikuwa lazima katiba isomeke; Katiba ya
CHADEMA ya Mwaka 2006; Toleo la 2014 kwa ajili ya kuingiza mabadiliko
ya kanuni (si katiba).
Maneno yanayosomeka juu ya cover (kama ilivyoboreshwa 2014 badala ya
TOLEO LA 2014), ni makosa ya mchapaji/uchapaji tu.
Hakuna mabadiliko ya Katiba ya Chama ya Mwaka 2006. Maana ili ufanye
mabadiliko ya Katiba kuna vikao vya kikatiba vinavyofanya kazi hiyo.
Vimeainishwa kwenye Katiba.
Watu wa CCM au mawakala wao hawawezi kutafsiri Katiba ya CHADEMA,
isipokuwa WanaChadema wenyewe. Ndiyo maana Wanachadema wanajua kuwa
Katiba ya Chama ya Mwaka 2006; Toleo la 2014 halina kifungu wala ibara
inayozungumzia Katibu Mkuu kuwa na mamlaka ya kuteua idadi yoyote,
wala mtu yeyote kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu.
Upatikanaji wa Wajumbe wa Vikao vya Chama umeelezewa na kufafanuliwa
vizuri kabisa ndani ya Katiba ya Mwaka 2006; Toleo la Mwaka 2014.
Haujabadilika.
Kupitia kitu kinachoitwa Open Chadema (maana CCM wameshindwa
kutekeleza Open Government badala yake Rais Kikwete anaishia
kuudanganya ulimwengu kuwa ifikapo Aprili mwaka huu bunge lingetunga
Sheria ya Kupata Taarifa), mtu yeyote anaweza kupata nakala ya katiba
ya chama, tena toleo hilo la 2014 ni very portable. Unaweza kuweka
hata kwenye mfuko wa shati au suruali....
BILION 53 ZA HATIFUNGANI KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI TANGA
-
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Hamidu Aweso(MB) ameipongeza Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) kwa ubunifu uliofanyika wa
uwekezaji wa...
4 hours ago
0 Comments:
Post a Comment