WAKAZI wa jiji la Arusha na viunga vyake jana walikumbwa na taharuki baada ya ndege moja inayoadhaniwa kuwa ni ya Jeshi la Wananchi, (JWTZ), kupita angani ikiwa juu kidogo ya majengo marefu tofauti na ndege nyingine huku ikitoa mngurumo mkubwa hivyo kusababisha baadhi ya wananchi kukimbia hovyo.
Hali hiyo ilitokea jana majira ya saa 7 mchana ambapo ndege hiyo ilipita mara mbili ikitokea upande wa Mashariki kuelekea magharibi ambapo ilirudi Mashariki na kurokome kabisa.
Tanzania Daima iliwashuhudia watu wakitoka mbio kwenye ofisi zao huku wale walio nje wakikimbilia ndani maeneo ya barabara ya Goliondoi .
Mariam juma aliyekuwa anapita na bidhaa zake za viatu vya mtumba alipata mshtuko na kukaa chini ambapo alimweleza mwandishi wa habari hizo kuwa alifikiri ni bomu na kwa kuwa hakuwa na pa kukimbilia akaona bora akae chini karibu na gari pengine atasalimika.
Mkazi mwingine wa jijini hapa, Lucas Urio, alisema kuwa yeye alikuwa anapata soda kwenye mgahawa mmoja amelazimika kutoka mbio baada ya kusikia mngurumo huo akidhani kuwa umepigwa bomu ambapo alipotoka nje ndiyo akaona ndege hiyo ikipita mara ya pili.
"Kwa kweli kama ningekuwa na ugonjwa wa moyo leo ningekufa kwa namna nilivyoshtuka, nilikuwa nakunywa soda nimeiacha mezani, sijawahi kuona hali kama hii, inatisha sana ule mngurumo ni mkubwa mno," alisema Urio.
Hata hivyo juhudi za Tanzania Daima kumpata Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.
Hata hivyo habari zaidi zinadai kuwa huenda ndege hiyo ni sehemu ya maandalizi ya JWTZ kuadhimisha miaka 50 tokea kuanzishwa kwake septemba 1, 1964.
AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAWATOA HOFU WATEJA WAKE WA KARIAKOO
-
Akiba Commercial Bank Plc imeendelea kujitoa si tu kuhudumia wateja wake
bali pia kushiriki katika juhudi za kijamii wakati wa dharura na majanga,
ikiwa ...
6 hours ago
0 Comments:
Post a Comment