Agnes Lucas, (28) enzi za uhai wake
Sent from my iPhone
MKAZI wa
Ilboru, Lucas Lomayan, anadaiwa kumuua mkewe, Agnes Lucas, (28), maarufu kama
Asha kwa kumpiga kichwani na kitu kizito na kumkata maeneo mbalimbali ya mwili
na kitu chenye ncha kali kisha kutoweka nyumbani kwao.
Inadaiwa Lomayan
ambaye hufanya kazi ya kuuza nyama ya ng’ombe kwenye bucha maeneo hayo aliwafungia
watoto wao sebuleni huku akiwatisha kwa rungu ili wasipige kelele ambapo
aliingia chumbani na kumpiga mkewe ambaye alikuwa akilia lakini majirani
hawakuweza kutoa msaada kwa madai kuwa ilikuwa ni mazoea yao kupigana mara kwa
mara.
Tukio hilo lililovuta
hisia za wengi jijini hapa lilitokea usiku wa kuamkia jana maeneo ya Ilboru karibu
na Kwa Mollel ambapo kwenye nyumba hiyo zinaishi familia tatu wakiwemo ndugu
wawili wa Lomayan na mpangaji mmoja.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo
bado hawajajua chanzo chake ila alidai kuwa kifo cha marehemu kimetokana na
kupigwa na kitu kizito kichwani na wanaendelea na juhudi za kumtafuta Lomayan.
WATOTO WA
MAREHEMU WANENA
Watoto wa
Marehemu, Jesca (10) na Jackson, (5) walisema kuwa baba yao alikuwa na tabia ya
kumpiga mama yao mara kwa mara ambapo amekuwa akiwakataza wasipige kelele vinginevyo
wakikaidi amekuwa akiwajeruhi.
Jackson
alisema kuwa kuna siku alipiga kelele
baba yake alimpiga kwa kutumia rungu kwenye mkono wa kushoto huku Jesca akidai
kuwa yeye kuna wakati aliwahi kupiga kelele baba yake akampiga na ubapa wa
panga mgongoni hali iliyomsababisha akapatiwe matibabu hospitali.
“Jana mama
alichelewa kuja alikuja kama saa nne usiku, alipokuja baba akafunga mlango
akaanza kumpiga, sisi tulikuwa tunalia taratibu, (anawaza kidogo) baba alikuja
kunywa maji kwenye friji akanigusa na rungu hapa kwenye shavu (la kushoto) Huyu
Jakson hakusikia alikuwa ameshalala.
“ Mama
alilia sana na mimi nikawa nalia kimyakimya mpaka nikapitiwa na usingizi,
nilipoamka asubuhi tukakuta baba hayupo ila mama yupo kitandani, nikabandika
chai nikaenda kumsalimia mama akawa haitiki ndiyo nikaenda kumuita mama Oscar,”
alisema Jesca.
Alisema kuwa
chumbani kwa wazazi wake kulikuwa kumetapakaa damu chini na kitandani alikokuwa
amelala mama yao.
MAJIRANI
WANENA
Mama Oscar
ambaye ni jirani wa marehemu aliyeolewa na kaka wa Lomayan, alisema kuwa
hakusikia wakati Lomayani akimpiga mkewe ila asubuhi watoto wa marehemu
walimuita wakimwambia kuwa wanamuita mama yao haitiki.
“Nilienda
nikamkuta amelala akielekea ukutani huku mwili wake ukiwa umevimba nilivyomuona
nilidhani anahitaji kupelekwa hospitali hivyo nikatoka nje nikawaita ndugu zetu
walipomuangalia wakabaini kuwa kashakufa,” alisema Mama Oscar ambaye alidai
kuwa haelewi chochote zaidi kwani baada ya hapo alipoteza fahamu.
Majirani
wengine waliongea kwa sharti la kutotajwa majina yao walisema kuwa Lomayan
amekuwa na tabia ya kumpiga na kumjeruhi mkewe kwa kumkata na panga mara kwa
mara ambapo walisema kuwa marehemu Agnes alikuwa ana alama mbili kubwa usoni
alizoshonwa baada ya kukatwa na mumewe siku za nyuma .
“Jana sisi
tulisikia kelele kama kuanzia saa tatu hivi usiku lakini hatukuamka kwa sababu
ni kawaida yao, sisi tunakaa kwa huku nyuma ya nyumba yao na ziliendelea mpaka
kwenye saa tisa usiku tukajua wameelewana wakaamua kulala” alisema jirani
huyyo.
Alisema kuwa
asubuhi waliposikia kuwa mama Jesca amefariki walifika kwenye nyumba hiyo na
kukuta damu zikiwa zimetapakaa chumbani nyingi zikiwa chini na nyingine
kitandani huku mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa na balnketi lakini walipomfunua
walikuta akiwa hana nguo hata moja huku ukiwa umevimba sana.
Jirani
mwingone alisema kuwa alipomuangalia marehemu alikuwa amebonyea kichwa eneo la
kisogoni na juu kidogo ya paji la uso ambapo alikuwa ametapaa damu kwenye
maeneo mbalimbali ya mwili hivyo ilimuia vigumu kubaini ni maeneo gani hasa
aliyojeruhiwa.
“Kila mtu
anatunyooshea kidople majirani kwa nini hatukusaidia lakini ukweli unajulikana
kabisa marehemu na mume wake kila wiki ni lazima wapigane na hata akijeruhiwa
anaenda kwao anakaa kidogo wanarudi na wakati mwingine hata kwao haendi
anachofanya anaenda hospitali anashinwa anarudi sasa tungeingiliaje kwa hali
kama hiyo?,” alihoji jirani mwingine.
MAMA WA
MAREHEMU ANENA
Mama wa
Marehemu, Jamillah Ramadhan, (48), alisema kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa
za kifo cha mwanae huyo wa kwanza kati ya watoto watatu aliokuwa nao huku
akidai kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Lomayan aliamua kumuua.
“Mara kwa
mara walikuwa akigombana wanayazungumza wanayamaliza wanarudi kulea watoto wao
sijui ni kitu gani kilimuongia huyu kijana mpaka kuamua kumuua mwanangu na
sijui nani atawalea hao watoto manake naye kakimbia,” alisema Jamilah huku
akilia.
Mmoja wa
ndugu wa marehemu alisema kuwa baada ya kupata taarifa walienda kumuona
marehemu Agnes kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mount Meru
ambapo walipomuangalia maeneo ya uso walimuona ana alama kichwani na katobolewa
na kitu chonye ncha kali juu ya mdomo na pana tundu.
Sent from my iPhone
0 Comments:
Post a Comment