WASHTAKIWA wanaosadikiwa kujihusisha na makundi ya kigaidi nchini,
ikiwemo kundi maarufu la Al-Shabab, wameiomba mahakama ielekeze
wapatiwe matibabu na wapewe fursa ya kuonana na ndugu zao kwani
wamekuwa wakizuiliwa kwa kipindi chote walipokuwa mahabusu kwenye
gereza la Kisongo.
Aidha wameomba mahakama hiyo iliagize jeshi la polisi kuleta
mahakamani hapo vitu vyao walivyowanyang'anya ikiwemo simu, hati za
kusafiria, nguo na viatu vyao ili ndugu zao wakavichukulie hapo
wanapoamini ni mahali salama zaidi.
Maombi hayo yalitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mustapher
Siyani, na washtakiwa nane kati ya 16 wanaokabiliwa na mashtaka 16 ya
kuua na kukusudia kuua.
Walisema kuwa kwa kipindi cha wiki mbili walichokuwa mahabusu
hawaruhusiwi kuonana na ndugu zao kwani wanapofika magereza kwa ajili
ya kuwaona huzuiliwa jambo linalowafanya wanakosa hata mahitaji muhimu
ikiwemo dawa ya kusafishia meno.
Pia walilalamika kuwa wanaumwa lakini hawapewi matibabu licha ya
kufikisha malalamiko yao kwa askari magereza waliodai kuwa wamekuwa
hawawasikilizi.
Madai hayo yalimsukuma hakimu, Siyani kumuita mmoja wa askari Magereza
aliyekuwa mahakamni hapo kutolea ufafanuzi juu ya sababu zinazopelekea
washtakiwa hao kunyimwa kuonana na ndugu zao.
Askari huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema
kuwa wapo katika hatua za mwisho za kuandaa utaratibu utakaofaa
kuwezesha washtakiwa hao kuonana na ndugu
zao, kulingana na mazingira ya kesi hiyo.
Akitolea uamuzi mdogo wa maombi hayo hakimu, Siyani aliosema kuwa
mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hivyo akawataka
washtakiwa hao kumwandikia barua mpelelezi wa shauri hilo wakimweleza
malalamiko yao.
"Orodhesheni madai yenu yote yeye ataoana kitu gani kinafaa mpewe au
la, na kama kinahusika katika kesi, suala kama la simu endapo kuna
ushahidi wa kuhusika na kesi haiwezekani mkapewa,"alisema hakimu huyo.
Aidha aliagiza washitakiwa hao Abdala Athumani, Swalehe Hamisi,Abdallah
Yasini,Hassani Saidi, Sudi Lusuma,Abdulkarim Hasia na Shaban Wawa
kupewa nakala ya hati ya mashitaka inayowakabili kila mmoja, sababu ni
haki yao ya msingi.
Kesi hiyo imeahirishwa na itarudi mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa
Juni 25 mwaka huu ambapo kwa siku ya jana Polisi waliimarisha ulinzi
kama ilivyokuwa siku ya kwanza kwa watuhumiwa hao kufikishwa
mahakamani hapo ambapo kulikuwa na ukaguzi wa mizigo na pochi
walizobeba watu walikuwa ndani ya viwanja vya mahakama.
Awali mahakama hiyo ilielezwa kuwa washtakiwa hao, walihusika na
tukio la milipuko ya mabomu katika maeneo ya Mianzini na Arusha
Night Park hivi karibuni.
Washtakiwa hao wanatuhumiwa kusajili na kusafirisha vijana kwenda
katika mafunzo maalum nje ya nchi kujifundisha masuala ya kigaidi na
kushawishi vijana katika maeneo mbalimbali ya nchi wakihusika ni kundi
la kigaidi la Al-Shabab la nchini Somalia, linaloendesha mauaji,
utekaji nyara, uvamizi ndani na nje ya nchi hiyo.
Mahakama hiyo ilielezwa kuwa kati ya mwaka 2010 hadi 2014, washtakiwa
hao walifanya kazi ya kushawishi na kusajili vijana kwa lengo la
kuwapeleka katika mafunzo maalum ya uhalifu katika nchi moja ambayo
jina limehifadhiwa kwa sasa.
Alidai katika muda huo walisajili vijana kutoka maeneo mbalimbali
nchini ambapo jitihada za uchunguzi kuwabaini wote waliosajiliwa
zinaendelea ili wakipatikana nao waunganishwe katika kesi hiyo.

0 Comments:
Post a Comment