Kamanda wa Polisi katika mji wa Mombasa nchini Kenya, Henry Ondiek amesema kuwa watu wasiojulikana wamemuuwa kwa risasi Sheikh Mohammed Idris, mwenyekiti wa Baraza la Maimam na Wahubiri wa Kiislamu nchini humo.
Sheikh huyo amepigwa risasi asubuhi hii akitoka kwenye msikiti, na ni kiongozi wa nne wa kiislamu kuuawa na watu wasiojulikana katika mji wa Mombasa. Mwezi Agosti mwaka 2012 Sheikh Aboud Rogo alipigwa risasi na kuuawa na mwaka mmoja baadaye kiongonzi mwingine wa kiislamu akauawa katika mazingira kama hayo.
Mwezi Aprili mwaka huu, sheikh mwingine Abubakar Sharrif Ahmed ambaye pia alijulikana kama Makaburi alipigwa risasi na kufa mbele ya msikiti. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameishutumu serikali ya Kenya kuwa nyuma ya mauaji hayo. Nchi hiyo inakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi, yanayoshukiwa kufanywa na wanamgambo wa kisomali wakisaidiwa na watu wanaowaunga mkono.
Source DW
JAB YAKEMEA UVUNJAJI WA SHERIA ZA AJIRA KATIKA SEKTA YA HABARI
-
*Na Mwandishi Wetu.*
*Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewasisitiza waajiri kwenye
vyombo vya habari nchini kuzingatia kikamilifu masharti ya...
3 hours ago
0 Comments:
Post a Comment