BARUA YA KIOFISI YAMUOKOA NAIBU MEYA KWENDA GEREZANI

NAIBU Meya wa jiji la Arusha, Prosper Msofe, amelazimika kuwasilisha mahakamani barua za shughuli ya kutiliana mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Singapori juu ya uandaaji wa mpango kamambe (Master Plan) wa majiji ya Arusha na Mwanza ili kushawishi kupewa dhamana.

Hayo yalitokea jana mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Arumeru, Jackson Ndaweka, aliyesikiliza shauri la ashambulio la kudhuru mwili linalomkabili Naibu Meya mara baada ya  wakili wa Serikali, Diaz Makule kutaka mshtakiwa huyo asipewe dhamana.

Msofe aliileza mahakama hiyo kuwa kwa shitaka linalomkabili lina dhamana anaomba adhaminiwe ili akahudhurie tukio hilo muhimu kwa mustakabali wa wananchi wa jiji la Arusha.

Alikabidhi barua hiyo kwa hakimu kama uthibitisho huku akiendelea kuweka msisitizo kuwa shughuli hiyo inafanyika kwenye ofisi yake na ujumbe wa watu kutoka nchini Singapori umeshaingia hivyo kama hatakuwepo itaadhiri shughuli hiyo na fedha za umma zitapotea bure.

Kwa upande wake wakili wa Serikali, Makule aliendelea kuweka msisitizo kuwa hakuna aliye juu ya sheria hivyo  Naibu Meya asipewe dhamana kwani ameendelea na matukio ya kupiga watu hata baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa kesi nyingine kama hiyo iliyokuwa mahakamani hapo wiki iliyopita.

Hakimu Ndaweka alilazimika kuahirisha shauri hilo kwa saa mbili ili atolee uamuzi hoja hizo ambapo majira ya saa 8:00 mchana alitolea uamuzi ambapo Naibu Meya huyo aliendelea kukaa chini ya ulinzi wa polisi.

Akitolea uamuzi suala hilo, Hakimu alisema ameamua kumuachia kwa dhamana Naibu Meya, Msofe baada ya kuridhika kuwa mashtaka yanayomkabili yana dhama na tukio analotuhumiwa la  kumpiga mgambo, Wiliam Molel  lilifanyika April 16, mwaka huu na si siku tatu baada ya Naibu Meya huyo kuachiwa kwa dhamana wiki iliyopita.

Awali mwanasheria wa serikali, Makule aliieleza mahakama hiyo kuwa April 16, mwaka huu akiwa maeneo ya Ngarenaro, Naibu Meya alimshambulia na kumjeruhi  mgambo, Mary Samwel ambapo alimchania nguo yake na brazia jambo lililomdhalilisha na ni kinyume cha sheria.

Shauri limeahirishwa mpaka julai, 14 mwaka huu litakaporudi mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa ambapo Naibu meya huyo hataruhusiwa kutoka nje ya jiji la Arusha bila ruhusa maalum ya mahakama.

0 Comments:

Post a Comment