13 WAFARIKI AJALINI SINGIDA



 hali ilivyokuwa kwenye eneo la tukio


WATU 13 wamefariki papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Noah kugongana uso kwa uso na gari kubwa la kukeba mizigo ambao dereva na utingo wake walitokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo.

Ajali hiyo imetokea saa tatu zilizopita eneo la Isuna mkoani Singida  ambapo waliofariki ni wale waliokuwa kwenye Noah  ikitokea Itigi.

Maiti  zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida. 

0 Comments:

Post a Comment