KAMA ambavyo jana umma wa Watanzania ulitaarifiwa kupitia kwenye
mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na wanahabari,
Chama leo kinaanza operesheni ya takriban wiki mbili kwa nchi nzima
(mijini na vijijini).
Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C-
Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo
zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu
tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.
Timu hizi zinajumuisha viongozi wakuu wa Chama, watendaji kutoka
Makao Makuu ya Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu, Viongozi wa Kanda, Mikoa,
Wilaya, Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji pamoja na wabunge wote wa
CHADEMA katika maeneo husika.
CHADEMA itatumia operesheni hii ya wiki mbili kuandaa umma wa Watanzania juu ya masuala…
MWENYEKITI wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema leo
wanaanza
Operesheni Pamoja Daima kwa takriban wiki mbili kwa nchi nzima (mijini na
vijijini).
Wamejigawa kwenye timu 6 kuendesha poeresheni hiyo ya M4C ambapo Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu
tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.
Timu hizi zinajumuisha viongozi wakuu wa Chama, watendaji kutoka
Makao Makuu ya Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu, Viongozi wa Kanda, Mikoa,
Wilaya, Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji pamoja na wabunge wote wa
CHADEMA katika maeneo husika.
CHADEMA itatumia operesheni hii kuuandaa umma wa Watanzania juu ya masuala kadhaa muhimu kwa hatma ya nchi yao kama ifuatavyo;
1. Mjadala wa rasimu ya pili ya katiba mpya- Bunge Maalum la Katiba Mpya
Wakati huu ambapo nchi Watanzania wanasubiri vikao vya Bunge Maalum la Katiba,
pamoja na Tume ya Warioba kufanya kazi nzuri kwa kukusanya na kuzingatia
maoni ya watu (ambayo CCM wanayapinga wakiweka mbele maslahi ya chama
chao badala ya Watanzania wenye nchi yao), bado kuna masuala ambayo;
(a) yanahitaji msisitizo yaendelee kubakia kwenye rasimu
(b) yanahitaji kuboreshwa
(c) yanahitajika kuongezwa kwa sababu hayamo
2. Kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni kuamua
Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Hii ni moja ya shughuli ya 'kufa na kupona' mwaka huu kwa sababu kuna
mamilioni ya Watanzania hadi sasa Serikali ya CCM imewanyima haki yao ya
kikatiba ya kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao, maendeleo yao kupitia kura.
3. Uchaguzi wa ndani ya chama ambao hadi sasa unaendelea katika ngazi ya msingi
nchi nzima hatimaye ngazi ya taifa.
4. Masuala ya Watanzania na umiliki wa rasilimali zao ambazo kwa sasa zinaonekana
kuwanufaisha wageni, watawala na watu wenye mahusiano na watawala, pia hali
ya ugumu wa maisha inayozidi kuwakabili wananchi ikiwa na uhusiano na uongozi
mbovu unaokumbatia ufisadi na sera zilizoshindwa, yatapewa kipaumbele kikubwa
katika ziara hii.
5. Bila kusahau kwamba 'all politics is local', hivyo chama kitatumia fursa hii
kuzungumza na wananchi juu ya kero mbalimbali zinazowakabili na CHADEMA
inaweza ku-offer nini. Na mengine kadha wa kadha yenye umuhimu kwa
maendeleo ya watu.
Ifuatayo ni ratiba ya leo na kesho kwa timu tatu za angani ambazo zinatumia usafiri wa helkopta 3;
Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa;
Mbambabay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo kisha kwa leo watamalizia Songea Mjini
Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Issa Saidi Mohamed
Nzega (Ndala), Igunga (Nkinga), Tabora Kaskazini (Mabama) na Tabora mjini
Timu ya Kamanda Tundu Lissu na John Heche
Lushoto, Korogwe, Muheza na Tanga mjini
*
Tutawapatia updates kadri muda unavyokwenda. Accounts za CHADEMA
mitandaoni ikihusisha pia 'vyombo' vya chama kama websites na blogs,
ndizo zitakuwa vyanzo rasmi vya taarifa za uhakika kwa kila
kinachoendelea field.
Tutashirikiana na mods pamoja na watu
wengine wote hasa walioko fields kwenye timu zote 6 kuhakikisha
Watanzania wanapata taarifa sahihi, za uhakika, kwa wakati, huku pia
tukiomba uvumilivu wenu na subira inapolazimika, ili kupata vitu vizuri
maana mikutano itafanyika maeneo ya vijijini na mijini.
Punde
tutatoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za watu kama vile, kwa nini helkopta
(tena idadi imeongezeka, hakuna chama cha siasa kiliwahi kufanya kama
hivi kwenye operesheni kama hii), kwa nini PAMOJA DAIMA (wengine
wanafikiri ni tofauti na M4C).
Kurugenzi ya Habari Chadema
NABII MKUU PROF. GEORDAVIE ATUNUKIWA CHEO CHA UPROFESSOR
-
*WAZIRI KABUDI AANGAZA UHUSIANO KATI YA ELIMU, AMANI NA USHIRIKIANO*
*Na Woinde Shizza, Arusha*
*Katika hafla ya kihistoria iliyofanyika katika Nyumba ...
53 minutes ago
0 Comments:
Post a Comment