WAENDESHA BODABODA ARUSHA WATAKA IGP AMWONDOE RTO KWA MADAI YA RUSHWA


WAENDESHA bodaboda wa jiji la Arusha wa memuomba mkuu wa jeshi la polisi (IGP),Ernest Mangu kuwaondoa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani (RTO) , mkaguzi wa polisi Daud mshana , na koplo Peter , ambao wamekuwa ni wasumbufu na vinara wa kuomba rushwa huku RTO, akidaiwa kukataa kuwasikiliza  na badala yake huwa anawafukuza wanaofika ofisini kwake .

Mwenyekiti wa umoja wa waendesha pikipiki (UWAPA),  Godlight Rugemalila, alisema  lengo la maandamano yao ya siku mbili ni kupinga vitendo vya jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani cha kuwabambikizia makosa na kuwatoza faini kubwa ,sanjari na kuwaomba rushwa .

kero nyingine ni pale wanapokamatwa na polisi pikipiki zao zinafungwa minyororo (Chain) na kupelekwa polisi kikosi cha usalama barabarani na kupata usumbufu kuzikomboa licha ya kulipa faini huzungushwa mpaka watoe rushwa .

Wamesema katika risala yao kuwa kero kubwa kuliko zote ni mkuu wa kikosi cha usalama bara barani, R.T.O,Marison Makyoma, ambae amekuwa  akiwalazimisha kutoa rushwa na kutumia ubabe na vitisho na pia amefuta vituo vya  maegesho ya pikipiki vilivyoidhinishwa na halmashauri ya jiji katika maeneo mengi .

Wametaka kuwepo dawati la boda boda kwenye kituo cha polisi ili kuweza kutatua matatizo yao na hivyo kuwaondolea usumbufu anaoupata sasa.

Wamesema boda boda ni mkombozi kwa wananchi zimetoa ajira kwa wengi na hivyo kupunguza uhalifu .

Wamesema katika jiji la Arusha kuna vituo 144 vya boda boda na vingine tayari vina uongozi na vingine vipo katika mchakato wa kukamilisha uongozi .

Katika maandamano hayo waendesha boda boda walikuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ikiwemo, 

"Tumechoshwa kufanywa ATM na jeshi la polisi, IGP ,Ernest mangu , muondoe R.T.O ni majanga Arusha,Hatutoki nasi ni watanzania tumechoshwa  kugeuzwa kuwa mashine za ATM, haya ni majanga


Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa wilaya ya Arusha, John Mongela ametoa amri ya kusitisha kwa wiki mbili oporesheni ya ukaguzi na ukamataji pikipiki hizo za kubeba abiria.

Alisema ametoa muda huo ili kuwawezesha wamiliki na madereva kukamisha taratibu na sheria za usalama barabarani ikiwemo madereva kuwa na leseni pamoja na kuwa na kofia maalum ya kuendesha vyombo hicvyo vya moto.


Hata hivyo operesheni ya kusaka pikipiki zote zinazojihusisha katika matukio ya uhalifu inaendelea bila kikomo katika maeneo yote ya wilaya ya Arusha lengo ni kudumuisha usalama katika vijiwe mbalimbali vya boda boda..

Mongela, amewaeleza waendesha pikipiki jijini Arusha kupitia Umoja wao waendesha pikipiki (UWAPA) kwenye uwanja wa mpira wa Sheik Amri Abeid Januari 15, mwaka huu.

Mongela amewaagiza waendesha bodaboda hao wawe na uongozi kila kijiwe ili kuwatambua waendesha pikipiki ambao sio waaminifu wanajihusisha na vitendo vya uhalifu ambao wanawaharibia sifa yao ya kutoa huduma ya usafiri.

Mongela, amba pia ni mlezi wa waendesha boda boda jijini Arusha, amewataka wasikubali kutoa rushwa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani badala yake wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria na watoe taarifa kwake au kwa mkuu wa polisi wa mkoa (RPC) na wilaya (OCD) pindi  akiombwa rushwa.

Amewataka wawe na vitambulisho , kuvaa vijamba koti (vizibao) maalumu ,sanjari na kuwa na kofia mbili moja kwa ajili ya abiria na kuhakikisha abiria wanavaa kofia hizo.






0 Comments:

Post a Comment