Hukumu ya ng'ombe wa Kapimilo kuharibu ekari 24 za mpungu, Oktoba 16

 

 


Na Mwandishi Wetu,

Mngeta


HUKUMU ya kesi ya uharibifu wa hekari 24 za shamba la mpunga inayomkabili, Mfugaji Kapimilo Kini, inatarajiwa kutolewa  Oktoba 16 mwaka huu katika Mahakama ya Mwanzo ya Mngeta, wilayani Mlimba, mkoani Morogoro.



Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mussa Kulita wa Mahakama ya Mwanzo Mngeta,  Kapimilo anayemiliki zaidi ya ng’ombe 10,000, anadaiwa kufanya uharibifu wa hekari 24 za mpunga kwa kuachia mifugo yake kufanya malisho ndani ya shamba la  Rashid Shaibu, kinyume cha sheria.


Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa mara ya kwanza Agosti 6 mwaka huu, tukio hilo lilitokea Juni 23,  majira ya jioni katika eneo la Chita ambapo ng'ombe wa Kapimilo wanadaiwa kufanya marisho katika shamba la Shaibu na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.


Hukumu ya kesi hiyo inayovuta hisia za wengi huko  katika kijiji cha Chita, imekuja baada ya  Mahakama hiyo chini ya Hakimu Mussa, kumaliza kusikiliza mashahidi wa upande wa mashitaka na  wa utetezi.


Mashahidi upande wa Mashitaka


Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo, Shaibu alidai kuwa katika vya usuluhishi vilivyofanyika katika ofisi ya Serikali ya Mtaa kwa nyakati tofauti, Kapimilo alikiri kosa na  alikuwa tayari kulipa fidia ya sh 400,000.


Alidai kwamba yeye (Shaibu) aligoma kupokea kiasi hicho cha fedha kwa sababu hakiendani na  hasara iliyosababishwa na ngo’mbe wa mshitakiwa walioteketeza zaidi ya hekari 24.


Aliongeza kuwa Kapimilo na familia yake,  walikiri pia hata  alama ya chapa waliyopigwa ng’ombe hao  ni yake,  lakini alipofika mahakamani hapo alikana kuwa sio wake.


Naye shahidi JOSEPH MBEVILE wa upande wa  mashitaka,  alidai kwamba tukio hilo lilitokea Juni 23 mwaka huu katika shamba la mpunga la Shaibu lililopo Mngeta, mkoani Morogoro.


Joseph ambaye ni mlinzi wa shamba  hilo na msaidizi wa Shaibu, alidai kuwa siku tukio alishuhudia kundi kubwa la ng'ombe wa Kapimilo wakifanya malisho katika shamba hilo kinyume cha sheria na aliwasilisha mahakamani hapo picha alizopiga za siku ya tukio hilo.


Shahidi mwingine, PHILBERT MAENDELEO ambaye ni BWANA SHAMBA, alidai kuwa alitumwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba kwenda kufanya tathimini kwenye shamba la Shaibu ili kujua ukubwa wa hasara iliyosababishwa na ng’ombe wa  Kapimilo.


Shshidi huyo alidai kuwa alikwenda kufanya tathimini hiyo tarehe 18, Julai mwaka huu na alibaini kuwa uharibifu uliofanyika katika  ni zaidi ya ekari 24.


Shahidi wa tatu upande wa mashitaka ni Mwenyekiti wa Kitongoji, MATHIAS MWAKAMI 


Shahidi huyo aliwasilisha barua mbalimbali Mahakamani zikionyesha kuwa awali  mfugaji huyo alikiri kosa na alitaka wakutane na mlalamikaji ili wamalize jambo hilo nje ya Mahakama.


Mwenyekiti huyo wa Kitongoji, aliendelea kueleza kuwa wawili hao walipokutana na kushindwa kuelewana, aliandika barua ya kutaka kesi hiyo iende Mahakamani


Mashahidi wa utetezi


Kwa upande wa utetezi, Kapimilo alianza  kutoa utetezi kwa kukana kwamba mifugo inayodaiwa kufanya malisho katika shamba la Shaibu, sio yake na hata alama ya chapa waliyonayo ng’ombe hao, sio yake.


Shahidi mwingine upande wa utetezi, Mahona Mwandu, alieleza mahakama kwamba  alipigiwa simu na mfugaji huyo ili aende kwa Mwenyekiti wa kitongoji kwani kuna malalamiko ya ng'ombe wake kulisha kwenye shamba la mpunga la Shaibu


Afisa Mifugo Kata ya Chita Lilian Kibira, ambaye ni shahidi upande wa utetezi,  alidai kuwa hatambui alama za ng'ombe hao kama ni wa Kapimilo Kini kwa sababu hakuna mfumo rasmi wa utambuzi wa mifugo toka wizarani. Hukumu ya kesi hiyo ni Oktoba 16.



0 Comments:

Post a Comment