PAPA LEO XIV ATOA WITO WA KUKOMESHA NA VITA TENA, AOMBA AMANI UKRAINE, GAZA NA KATI YA INDIA NA PAKISTAN

VATICAN



Papa Leo XIV ametoa wito mzito wa "kutokuwa na vita tena" kwa mataifa yenye nguvu duniani, akihimiza juhudi za kuhakikisha "amani ya kudumu" katika maeneo yanayokumbwa na migogoro duniani.

Katika hotuba yake ya Jumapili ya kwanza kama kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Leo alisema: "Natoa wito kwa mataifa yenye nguvu: kutokuwa na vita tena!"

Akitafakari juu ya hali tete katika maeneo mbalimbali, aliangazia vita vya Ukraine, mapigano yanayoendelea Gaza, na mvutano kati ya India na Pakistan.

Kuhusu Ukraine, alisema anaitakia "amani ya kweli na ya kudumu."

Kuhusu Gaza, alieleza kuguswa kwake kwa undani na hali ya kibinadamu: "Niliumizwa sana na matukio ya Gaza."

Kwa mvutano kati ya India na Pakistan, alikaribisha makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano na kusema: "Nina matumaini ya makubaliano ya kudumu kati ya India na Pakistan."

Papa Leo pia aliongoza sala ya Regina Caeli, kwa heshima ya Bikira Maria, mbele ya umati mkubwa uliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Papa Leo XIV alichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki siku ya Alhamisi, kufuatia kongamano la siku mbili lililofanyika mjini Vatican baada ya kifo cha mtangulizi wake, Papa Francis.


0 Comments:

Post a Comment