Majimbo Mapya Yatangazwa kwa Uchaguzi Mkuu 2025, Yafikia 272

 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ongezeko la majimbo ya uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo majimbo nane mapya yameongezwa, yakiwemo Jimbo la Ilongero na mengine kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.

Majimbo mapya yaliyotangazwa ni pamoja na Jimbo la Manyoni Magharibi kugawanywa na kuzaa Jimbo la Itigi, Jimbo la Singida Mashariki kuwa Jimbo la Ikungi Mashariki, Jimbo la Singida Magharibi kuwa Jimbo la Ikungi Magharibi, Jimbo la Tabora Kaskazini kuwa Jimbo la Uyui, na Jimbo la Handeni Vijijini kuwa Jimbo la Handeni.



Akizungumza na vyombo vya habari, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele, amesema:
"Kutokana na ongezeko hilo la majimbo nane, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano. Kati ya majimbo hayo 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar."



Akiendelea kufafanua kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Mwambegele aliongeza:
"Kutakuwa na kata 3,960 zitakazofanya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025."

Uamuzi huu unalenga kuhakikisha uwakilishi wa wananchi unaboreshwa kutokana na ongezeko la watu na mahitaji ya uwakilishi wa karibu zaidi kutoka kwa wabunge na madiwani.


0 Comments:

Post a Comment