TANAPA Yakabidhiwa Tuzo ya Mdhamini Mkuu kwa Mchango wa Kipekee Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere

 


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limepewa tuzo ya Mdhamini Mkuu na kutambua mchango wake mkubwa katika kufanikisha Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 103 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.



Tuzo hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, na kupokelewa  na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Musa Nassoro Kuji. Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo imefanyika , Aprili 13, 2025, katika Ukumbi wa Dkt. Jakaya Kikwete uliopo Jijini Dodoma.



Katika hotuba yake, Dkt. Mpango alilishukuru Shirika la TANAPA kwa kuonesha uzalendo na moyo wa kujitoa katika kushiriki shughuli za kitaifa, hasa zile zinazohusiana na kumuenzi mwasisi wa taifa.



TANAPA ni miongoni mwa taasisi mbalimbali zilizotoa msaada na kushiriki kwa karibu katika maandalizi na utekelezaji wa kumbukizi hiyo muhimu ya kitaifa.



0 Comments:

Post a Comment