Vyombo vya habari nchini Yemen vimeripoti kwamba jeshi la Marekani limefanya mashambulizi 10 kwenye maeneo ya mji mkuu wa Yemen, Sanaa, na mji wa bandari wa Hodeidah, hii leo.
Marekani ilianzisha wimbi jipya la mashambulizi katika maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran, ambao walisema wiki iliyopita kwamba wangelianzisha tena mashambulizi dhidi ya meli za Marekani katika Bahari ya Shamu ili kuunga mkono Wapalestina wanaoshambuliwa kwenye Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa kundi la wanamgambo wa Houthi amesema leo kwamba wamefanya mashambulizi mapya manne kwenye meli za kivita za Marekani katika Bahari ya Shamu. "Leo, tumeshambulia meli za kivita za Marekani katika Bahari ya Shamu kwa kujibu vitendo vyao vya kisasa na kinyume cha sheria vinavyofanywa dhidi ya watu wetu," alisema msemaji wa Houthi.
Marekani haijaweka wazi kuhusu maafa au athari za mashambulizi yake, lakini inasisitiza kwamba mashambulizi hayo ni sehemu ya juhudi za kujilinda dhidi ya tishio linalotokana na kundi la Houthi.
0 Comments:
Post a Comment