Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) uliofanyika kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 16 Februari, 2025.
Katika mkutano huo, Rais Samia alifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Rais wa Kenya, William Ruto. Alieleza kuwa, "Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya nchi za Afrika ili kukabiliana nayo kwa ufanisi."
Aidha, Rais Samia aliongoza Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kwa niaba ya Mwenyekiti wa AU, Rais wa Angola, João Lourenço, uliofanyika katika ukumbi wa Nelson Mandela, Makao Makuu ya Umoja wa Afrika.
Tanzania pia ilichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Umoja wa Afrika (Bureau of the African Union Assembly) kwa mwaka 2025, jambo ambalo ni heshima kubwa kwa taifa letu.




0 Comments:
Post a Comment