WATANO WAFARIKI, ZAIDI YA 40 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA KUPOROMOKA KWA GHOROFA KARIAKOO

 



Watu watano wamefariki dunia na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika tukio la kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam. 



Shughuli za uokoaji zinaendelea kwa ushirikiano wa wananchi na vyombo vya dola, ikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.



Kulingana na mashuhuda, ghorofa hiyo ilikumbwa na ajali majira ya saa tatu asubuhi wakati mafundi wa ujenzi walipokuwa wakifanya kazi ya kuongeza maduka. 



Hofu ipo kwamba idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka.


Msemaji wa Jeshi la Zimamoto, Naibu Kamishna Puyo Nzalayaimisi, alisema: "Tunawasihi wananchi kutulia kwani tupo imara na tunaendelea na jitihada za uokoaji kwa kushirikiana na vyombo vingine."


Wahanga waliokolewa wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu. 


Prof. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, alithibitisha kuwa majeruhi wote walipata huduma na kwa sasa, majeruhi saba ndio waliobaki.




Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia na wananchi waliathirika na mkasa huo.


Awali majira ya mchana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alithibitisha kutokea kwa kifo cha mtu mmoja na wengine 28 kuokolewa wakiwa wamejeruhiwa katika ajali ya kuporomoka kwa ghorofa iliyotokea asubuhi ya leo, Novemba 16 Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye eneo la ajali, Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia kwa vikosi vya uokoaji itahakikisha shughuli hiyo inafanyika mpaka watu wote waliokuwepo kwenye jengo hilo wakati wa ajali wanathibitika iwapo wako hai au wamefariki.


Shughuli ya uokoaji inaendelea katika kifusi cha ghorofa hilo lililokuw akatika makutano ya mtaa wa Kongo na Mchikichi.

0 Comments:

Post a Comment