MAFURU AFARIKI RAIS SAMIA ATUMA POLE KWA FAMILIA



Rais Samia Suluhu Hassan ameandika kwenye X kwamba amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024, katika hospitali ya Apollo nchini India.


Rais Samia alitoa pole kwa familia ya marehemu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Alisema Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu aliouonyesha katika nafasi mbalimbali za utumishi wa umma.


Rais Samia alimuombea Mwenyezi Mungu amjalie familia yake subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

0 Comments:

Post a Comment