TTCL KUUNGANISHA WILAYA ZOTE KWANYE MKONGO WA TAIFA NYUMBA KUMENOGA

 


Na Prisca Libaga ,Arusha.


Mkurugenzi Ufundi wa Shirika la mawasiliano Nchini TTCL mhandisi Cecil  Francis ,kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TTCL ,amesema wilaya 33 kati ya 139 ambazo hazijaunganishwa kwenye mkongo wa taifa zitaunganishwa mwaka huu na wakandarasi wanaendelea na kazi hiyo.



Ameyasema hayo Septemba 18 alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari kwenye kongamano la siku mbili la Wadau wa huduma za mtandao wa mawasiliano kwenye hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha .


Amesema kuwa TTCL inafanya kazi ya kuhakikisha nchi inaongea kwa kuunganisha mkoa kwa mkoa ,Wilaya kwa Wilaya ambapo tayari wilaya 106 zimeshaunganishwa kwenye mkongo wa taifa.



Amesema kuwa mkongo huo wa taifa wa mawasiliano unaojengwa unapita kila mahali ukiwa na ubora kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchina ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano ambao umeunganishwa na mkongo wa bahari ambayo ndio inatupa Internet.


Mhandisi Francis amesema Shirika hilo lina dhamana kubwa ya kutoa huduma bora za mawasiliano kupitia mkongo wa taifa  ambao ulianza kutekeleza mwaka 2013.


Amesema kuwa wameunda mkongo huo na nchi jirani za Kenya, Uganda ,Rwanda, Burundi ,Zambia, Malawi na kuna maunganusho yanayoenda kwenye mpaka na Msumbijina sasa wanaanza kushughulikia maunganusho na nchi ya DRC Congo, kupitia ziwa Tanganyika hadi mji wa Kalemii Nchini DRC.



Ameongeza kuwa pia TTCL inashugulikia maunganisho  kwenda kwenye kituo  kilichopo baharini hadi Mombasa Nchini Kenya.


Amesema TTCL inaendelea kutoa mchango wa mawasiliano kuhakikisha mkongo unaojengwa inakuwa na ubora wa hali ya juu kwa lengo la kufikisha huduma  kwa Wananchi na kupunguza gharama.


Mhandisi, Francis,amesema nchi yetu ni kiunganishi kikuu cha Mawasiliano kwenye ukanda wetu wa nchi za EAC na SADC.



0 Comments:

Post a Comment