SERIKALI YAOMBWA KUWEZESHA BAJETI KWA AJILI YA KUTAFSIRI VITABU KWA LUGHA YA ALAMA KWA AJILI YA WATOTO VIZIWI.

 

Happy Lazaro,Arusha .





Watoto wenye mahitaji maalumu hususani wasiosikia (viziwi)  wanakabiliwa na changamoto  ya kutokuelewa  darasani na kuishia kufeli kutokana na walimu wengi wanapofundisha  kutokutumia lugha ya alama.



Aidha changamoto  hiyo imekuwa ikipelekea kiwango cha kufeli kwa watoto hao kuendelea kuwa juu kutokana na kutokuelewa  chochote wanapokuwa darasani na hata kwa wazazi wake pia.




Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi  inayotafsiri maandishi mbalimbali kwa lugha ya alama (BILAT)  (TSLTDO )  Sensor Msimbete wakati akizungumza  na waandishi wa habari katika uzinduzi wa maadhimisho  ya miaka 30 ya elimu jumuishi  iliyofanyika  mkoani Arusha .




Msimbete amesema kuwa changamoto hiyo huchangiwa   na baadhi ya walimu wanaowafundisha  pamoja na wazazi wanaoishi nao kutokufahamu lugha za alama kwani mtoto anatakiwa pindi anapozaliwa anakutana na lugha hizo akiwa mdogo ili aweze  kuzoea  mazingira.


"Changamoto hizo zote wanazopitia wenzetu tunazijua kwani  na sisi tumepitia humo ndio maana tumeamua kuja na taasisi hii inayotafsiri maandishi  mbalimbali  kwa lugha ya alama BILAT (TSLTDO) kupitia programu ya BLOOM ambayo tumeanzisha sisi  ili kuwezesha watoto hao waliopo  ngazi ya chekechea  hadi chuo kikuu waweze kupata elimu wanayostaili kwa kutumia vitabu mbalimbali vilivyotafsiriwa kwa kutumia  lugha ya alama na kuweza kujitegemea baadaye na imeonyesha mafanikio   makubwa sana kwa viziwi "amesema Msembete. 


Aidha amefafanua zaidi kuwa,ni jukumu la.serikali kuwapatia bajeti kwa ajili ya kuendelea na zoezi hilo la kutafsiri vitabu mbalimbali kwa lugha ya alama ili  viweze  kusambazwa  mashuleni na vyuoni na hivyo kuwawezesha wanafunzi hao kuweza kuelewa  zaidi na kuongeza  kiwango cha ufaulu mashuleni.



"Hadi sasa hivi tumeshatafsiri vitabu sita ambavyo vitaweza kutumika katika elimu.ya chekechea  ambapo tumekuwa tukitumia programu  ya  BLOOM  katika  kufanya kazi hiyo na lengo ni kutafsiri  kuanzia elimu.ya awali hadi vyuo vikuu ila tunaomba serikali itupatie  bajeti kwa ajili ya kuendelea  na shughuli hiyo ili na wenzetu waweze kuelewa madarasa kupitia vitabu hivyo "amesema Msimbete.









 

0 Comments:

Post a Comment