Profesa Ndakidemi Ashiriki Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa na Kuomba Utekelezaji wa Ahadi za Ujenzi wa Barabara

Na Gift Mongi, Moshi


 

Mbunge wa Moshi Vijijini  Profesa Patrick Ndakidemi leo t ameungana na mamia ya wananchi wa jimbo la Moshi Vijijini  na jimbo la Vunjo katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr. Emanuel Nchimbi, pamoja na  Katibu Itikadi na Uenezi Na Mafunzo CCM taifa  Comrade Amos Gabriel Makala, Katibu wa NEC Organaizesheni ndugu  Issa Gavu, na Rabia Abdallah Hamid Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa Kimataifa. 



Akizungumza katika eneo la Njia Panda, Prof Ndakidemi  alieleza kuwa hadi kufikia Desemba 2023 jimbo  la Moshi Vijijini lilishapata miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 42. 


Alimshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa miradi iliyokuja katika Kata zote 16 za Jimbo la Moshi vijijini. 


Aidha alimueleza katibu Mkuu kuwa changamoto kubwa inayoikabili Jimbo lake ni ubovu wa  barabara. 



Alisema, barabara hizo hazitengenezwi kwa wakati zikiwemo zile zilizoko katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na ahadi mbalimbali za viongozi. 


Amemwomba Katibu Mkuu kuhimiza utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo kama ilivyoahidiwa kwenye ilani ya CCM na ahadi za viongozi wakuu.


 Aliomba kwa kuwa TARURA na TANROADS wana mambo mengi, basi fedha inayotolewa na TANAPA kwa maendeleo ya jamii (Corporate Social Responsibility) itumike kuzijenga barabara zilizoko katika vijiji vyote vinavyopakana na mlima Kilimanjaro katika wilaya za Siha, Hai, Moshi na Rombo



0 Comments:

Post a Comment