Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, afariki dunia wakati akijifungua
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dr. Shogo Richard Mlozi, amefariki dunia leo alfajiri wakati akijifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.
Chuo cha Uhasibu Arusha wametoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Eliamani Sedoyeka, ambaye ni mume wa mbunge huyo.
Aidha Katibu wa Bunge la EALA Alex Obatre amewaandikia wabunge wa bunge hilo kuwajulisha msiba huo mzito huku akiwataarifu kuwa kutakuwa na mkutano maluum kwa heshima ya mbunge huyo.
Habari hii imesababisha mshtuko mkubwa kwa jamii ya kisiasa na wananchi kwa ujumla, huku wakielezea masikitiko yao kufuatia kifo cha ghafla cha mbunge huyo.



0 Comments:
Post a Comment