KAMPUNI ya kimataifa ya Be Foward inaongoza kwa kuuza magari hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo kwa mwezi hupitisha wastani wa kati ya magari 6,000 na 10,000.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji hiyo hapa nchini, Daniel Japhet wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea banda lao likipo kwenye maonyesho ya wiki ya usalama barabarani kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
"Kwa mwezi kwa bandari ya Dar es Salaam zinaingia magari si chini ya 8,000 mpaka 10,000 kutegemea na msimu ambapo kuna yanayobaki nchini na mengine yanaenda nchi za jirani za Zambia, Zimbabwe, Malawi," anasema Daniel na kuongeza.
...Tunajivunia kuuza bidhaa bora, kwa ukweli na uwazi. Tunachokionyesha kwenye mtandao wetu ndicho kitakachomfikia mteja wetu hakuna biashara ya 'longolongo' wala wizi.
...Tuko wawazi na tunajivunia kuwa kampuni ya kimataifa ambayo tumekuwa kileleni kwa muda mrefu kwenye uuzaji magari,".
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Be Forward, nchini, amewataka watumiaji wa magari yao waendelee kuwaamini wao kama Be Forward lakini watii sheria za barabarani bila shuruti ili kupunguza vifo na ajali ambazo zinaweza kuepukika.
"Tumeshirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa kushiriki na kudhamini kwenye maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani kwa kutoa elimu na vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbali vya kuhamasisha watumiaji wa barabara kutii sheria bila shuruti na wao wenyewe kujihami na matumizi bora ya barabara," anasema Daniel na kuongeza
...Sisi kama wauzaji wakubwa wa magari tunajivunia kwa kuongoza kwa kuuza idadi kubwa ya magari Tanzania na Afrika Mashariki na Kati.
...Tumeona tushirikiane na serikali kwa kutoa sehemu ya faida yetu tudhamini wiki ya nenda kwa usalama katika kuelimisha watumiaji wa magari na barabara kama sehemu ya kusaidia jamii,".
Maonyesho hayo ya wiki ya wiki ya usalama barabarani yamezinduliwa leo Novemba 23,2021 na Rais, Samia Suluhu Hassan ambapo kauli mbiu ni "Jali maisha yako na ya wengine barabarani".
0 Comments:
Post a Comment