TCAA Yaruhusu Tena Safari za KQ Kutua Dar es Salaam

 TCAA Yaruhusu Tena Safari za KQ Kutua Dar es Salaam 



Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeruhusu tena Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuendesha safari za abiria kati ya Nairobi na Dar es Salaam, ikizingatia Haki za Uhuru wa Trafiki. Hatua hii inafuatia uamuzi wa Mamlaka ya Anga ya Jamhuri ya Kenya kukubali ombi la Tanzania kuruhusu Kenya kusafirisha mizigo yao kupitia Kampuni ya Air Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, amethibitisha uamuzi huo na kusema kuwa wamefikia makubaliano hayo baada ya mazungumzo ya kidiplomasia.


Jana, TCAA ilikuwa imetangaza zuio la KQ kutua Tanzania, lakini baadaye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, alithibitisha mazungumzo kati yake na mwenzake wa Kenya, Musalia Mudavadi, kuhusu suala hilo. Makubaliano hayo yanatarajiwa kurejesha tena uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya katika sekta ya anga.

0 Comments:

Post a Comment