TUWEKE MPANGO MKAKATI KUPAMBANA NA SHIDA YA MAJI...'Prof Ndakidemi'

 
TUWEKE MPANGO MKAKATI KUPAMBANA NA SHIDA YA MAJI...'Prof Ndakidemi'



Na Gift Mongi

Dodoma


Serikali kupitia wizara ya maji imetakiwa kuweka mpango kazi ili kupambana na upungufu wa maji unaotarajiwa kuja kwa takribani miaka kumi ijayo.



 Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi alitoa kauli hiyo bungeni ambapo alisema kuwa, katika hotuba ya Waziri wa Maji, Jumaa Awesso ameonyesha miaka 10 ijayo kutakuwa na upungufu wa maji kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na pia matumizi mabaya ya vyanzo vya maji. 



Kwa kujibu wa Prof Ndakidemi ni  kuwa, takwimu kuwa tutatumia mita za ujazo 883 badala ya 2105 ambazo zinatumika sasa hivyo inaonyesha kuwa miaka 10 ijayo kutakuwa na shida ya maji na hii imeanza kujionyesha kwani kwenye maeneo  mengi hapa nchini maji hupatikana kwa mgao na maeneo mengine hakuna kabisa 



Kadhalika aliiomba wizara kufanya kitu ambacho kitasaidia kutatua tatizo hilo kwani wasipofanya hivyo watakuwa hawajalitendea haki taifa na wananchi wake kiujumla



"Naomba niseme kitu hapa na ushauri kwa serikali  kuja na mpango kazi wa maji wa Taifa badala ya mikoa mitatu waliyoitaja ya Dodoma, Njombe na Rukwa kwa sababu tatizo hili ni la kitaifa hivyo washirikishe mikoa yote kujua vyanzo vya maji viko wapi kwa kutumia teknolojia na kujua maji yatapatikana wapi" Anasema Prof. Ndakidemi. 



Na kuongeza " Pia kujua mahitaji halisi ya maji na pia kujua makisio ya fedha ya siku zajazo na kuja na mkakati wa kutunza vyanzo ili shida itakayokuja miaka 10 ijayo tuanze kushughulikia sasa ".



Aliitaka Wizara kuishirikisha jamii kutengeneza mpango kazi huo wa maji ili jamii iwe sehemu ya hiyo na isije kuleta fujo ya kusema chanzo hiki ni mali yao.



Mbunge huyo aliitaka Serikali kuja na maoteo ya fedha itakayokidhi matakwa na ushauri utakaotokana na mpango kazi huo wa maji wa Taifa. 



Katika hatua nyingine, Ndakidemi aliishukuru Serikali kwa kutoa milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji katika kata ya Kimochi ambapo kumejengwa matanki mawili katika kijiji cha Liakombila. 



Alisema kuwa, kwenye chanzo kunabomba za nchi tatu hali inayopelekea maji kutotosheleza ambapo katika vijiji vya Mdawi, Sango wananchi wapatao 14000 hawajapata maji na kuomba Wizara kutatua changamoto hiyo. 



Pia alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa visima vitano na na kudai kuwa ameshaongea na Waandisi kwa ajili ya kujua visima hivo vitachimbwa sehemu gani. 



0 Comments:

Post a Comment