Na Gift Mongi
Moshi
Uwakilishi ni vitendo,naam ndiyo inavyofanyika katika jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kupitia mbunge wake Prof Patrick Ndakidemi'.
Prof Ndakidemi licha ya kucheza pande zote kama 'PELLE' ameweza kuunganisha jamii iliyomuamini kama kiranja mpambanaji.
Prof Ndakidemi ndiye aliyeanzisha mchakato na hatimaye upatinaji wa hospitali ya wilaya ya Moshi jambo ambalo halikuwepo tangu enzi na enzi!
Katika kuonyesha ukaribu na jamii
Prof Patrick Ndakidemi akiwa bungeni alisema kuwa, katika hotuba ya Waziri wa Maji, Jumaa Awesso ameonyesha miaka 10 ijayo kutakuwa na upungufu wa maji kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na pia matumizi mabaya ya vyanzo vya maji.
Kwa kujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa, takwimu kuwa tutatumia mita za ujazo 883 badala ya 2105 ambazo zinatumika sasa hivyo inaonyesha kuwa miaka 10 ijayo kutakuwa na shida ya maji na hii imeanza kujionyesha kwani kwenye maeneo mengi hapa nchini maji hupatikana kwa mgao na maeneo mengine hakuna kabisa
Hiyo ni hatua ya kwanza kwa Profesa huyo lakini michango yake bungeni inaenda mbali zaidi .
Akiwa katika ibada ya mazishi ya watu wanne wa familia moja waliofariki kwa kuangukiwa na nyumba yaliyofanyika katika kata ya Kimochi jimbo la Moshi Vijijini Prof Ndakidemi alitoa ahadi ya kuchangia milioni tano
"Kiasi hiki kinaenda kuleta faraja kama ubani lakini kurejesha makazi baada yao kuanguka hivyo kuongeza ugumu wa maisha"anasema
Prof Ndakidemi pia alitoa tani mbili za mahidi kwa wananchi wa kata za Mabogini na Arusha chini ambazo ziliathiriwa na mafuriko hayo.
Zaidi ya watu 4,000 wameripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo yaliyosabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Hata hivyo kaya 906 zimeathiriwa na mafuriko hayo huku watu sita wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo.
Hiyo ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Zephania Sumaye April 29,2024 Mjini Mosh wakati akipokea Misaada ya kijamii kutoka kwa msamaria mmoja kwa ajili ya wahanga wa mafuriko hayo waliopatiwa hifadhi kwenye shule ya Sekondari ya kutwa ya Lucy Lameck.

0 Comments:
Post a Comment