Mahakama ya IRMCT Yatangaza Kifo cha Washukiwa wa Mauaji ya Kimbari Rwanda Kabla ya Kukamatwa"

 Mahakama ya IRMCT Yatangaza Kifo cha Washukiwa wa Mauaji ya Kimbari Rwanda Kabla ya Kukamatwa"



Mwendesha mashitaka wa kitengo kilichokuwa kinasikiliza kesi zilizoachwa na mahakama ya Arusha alitangaza kuwa wale wote waliokuwa wakitafutwa na kitengo hiki kwa makosa ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda wote walifariki dunia.


Ametangaza hayo baada ya kubaini kwa uhakika kuwa wawili kati yao walikuwa bado wanatafutwa pia nao waliaga dunia.


Chombo hiki kinachojulikana kama International Residual Mechanism for Criminal Tribunals (IRMCT) kilitangaza kwamba uchunguzi wake "ulipata ushahidi" kwambawaliokuwa wamesali wote wawili Ryandikayo na Charles Sikubwabo walifariki mwaka 1998.


Sikubwabo alikuwa mwanajeshi wa zamani katika jeshi la Rwanda kulingana na chombo hicho baadae alikuwa mkuu wa wilaya ya Gishyita magharibi mwa Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari.


Alishutumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuhamasisha wanamgambo Interahamwe kuwaua Watutsi waliokuwa wamekimbilia makanisani, hospitali na majengo mengine ya umma.


Kwa mjibu wa IRMCT, Sikubwabo alikimbilia Zaire na kuelendelea hadi Kongo-Brazzaville, na Afrika ya Kati, kabla ya kuwasili Chad karibu 1997.


Na kwamba "uchunguzi wa kina" unathibitisha kwamba Sikubwabo alifariki dunia mjini N'Djamena mnamo 1998 na akazikwa huko katika hafla iliyohudhuriwa na watu wachache. Kaburi lake halikuwekwa alama naliliharibiwa na mafuriko baadaye.


Chombo hiki cha mahakama kilitangaza kwamba Ryandikayo, ambaye alikuwa mmiliki wa mgahawa na kiwanda cha matofali nyumbani kwake magharibi mwa Rwanda, pia alishtakiwa kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari aliyoyafanya katika wilaya ya Gishyita.


Yeye pia alikimbilia Zaire ya zamani katika kambi ya Kashusha, ambako alijiunga na kundi la waasi waFDLR, lakini baadaye akaenda Kinshasa ambako chombo cha mahakama hii kinasemakuwa uchunguzi wake unathibitisha kuwa huko ndiko alikofariki mwaka 1998 kutokana na ugonjwa.


Wawili hawa ndio wa mwisho waliokuwa wakisakwa na mahakama hii ya kimataifa kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari katika mchakato ulioanzishwa na iliyokuwa Mahakama ya Arusha.


Katika tangazo la IRMCT, mwendesha mashtaka wake Serge Brammertz alisema "kazi ya muda mrefu ilikuwa kujua walipo na kuwakamata."


Brammertz, hata hivyo, anakumbusha kwamba kuna zaidi ya watu wengine 1,000 wanaosakwa na mahakama za Rwanda kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari.


Anasema kuwa kazi ya haki dhidi ya mauaji ya kimbari itakamilika kwa mafanikio “ikiwa wahusika wote watafikishwa mahakamani.


Miongoni mwa watu 93 waliofunguliwa mashitaka na iliyokuwa mahakama ya Arusha, wapo waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka, Ryandikayo na Sikubwabo ndio walikuwa hawajakamatwa wala hatma yao kujulikana

0 Comments:

Post a Comment