HOSPITALI YA WILAYA YA MOSHI VIJIJINI KUKAMILIKA KATIKA MWAKA UJAO WA FEDHA
Na Gift Mongi, Dodoma.
Ni matumaini sasa kuwa uhakika wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Moshi Vijijini utaenda kukamilika mapema mwaka ujao wa fedha na kuleta ahueni kwa wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.
Wananchi wengi hususan wanaotoka ukanda wa juu walilazimika kupata huduma za matibabu katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi baada ya kukosekana kwa hospitali ya wilaya.
Kutokana na hali hiyo serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikaridhia kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika kata ya Mabogini ambapo swali zimetolewa shilingi millioni 500.
Katika mwaka ujao wa fedha 2024/2025 serikali imetenga kiasi cha bilioni 43.84 ili kumalizia viporo vya ujenzi wa hospitali za halmashauri mbalimbali nchini
Kauli hii ya serikali imetolewa leo bungeni mei 15 na naibu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Zainab Katimba waki akijibu swali la nyongeza lililotelekezwa kwake na mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi
Aidha katika swali la msingi Prof Patrick Ndakidemi aliuliza swali kama ifuatavyo
Je? Serikali ina mipango gani ya kumalizia ujenzi wa Hospitali ya wilaya inayojengwa Mabogini katika jimbo la Moshi vijijini?
Angalia Video
0 Comments:
Post a Comment