MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imefuta rufaa iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake watano baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, kuwasilisha ombi la kuiondoa Rufaa hiyo namba 155/2022 .Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Sabaya akitoka mahakamani akiwa ameambatana na wakili wake, Moses Mahuna mara
Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi ya Uhujumu uchumi namba 27/2021 katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha ambapo uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi, Dkt Patricia Kisinda.
Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Mfululizo Mahakama kuu Kanda ya Arusha kuanzia Aprili 29, 2024 mpaka Mei 03, 2024 mbele ya Jaji, Salma Maghimbi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo.
Akiwasilisha nia Ya kuliondoa shauri hilo mbele ya Jaji Salma, wakili wa serikali Akisa mhando aliieleza mahakama hiyo upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na rufaa hiyo dhidi ya Sabaya
“Mhe Jaji, Shauri hili limekuja kwa ajili ya kusikilizwa ,hata hivyo mrufani (Jamhuri) imewasilisha ombi chini ya kifungu cha sheria No.386 (1) cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022,ombi letu ni kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na Rufaa hii dhidi ya Sabaya na wenzake,hivyo tunaomba kuiondoa hapa mahakamani," Mhando aliomba mahakamani japo.
Upande wa wajibu rufaa hawakuwa na pingamizi juu ya ombi hilo hivyo Jaji Maghimbi alitoa uamuzi kwamba rufaa hiyo imeondolewa mahakamani rasmi.
Kufuatia uamuzi huo, sabaya anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi leo safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia Juni 2,2021 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.
Wakili wa sabaya,Moses Mahuna mbele ya waandishi wa habari ameeleza kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe, hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana rasmi na Mahakama.
0 Comments:
Post a Comment