Vuta nikuvute Israel, Iran

Vuta nikuvute Israel, Iran 



Baraza la mawaziri la vita la Israel limekutana kujadili jinsi itakavyojibu mashambulizi ya Iran ya droni na makombora.


Kwa upande wa Iran inasema itajibu ikiwa Israel itaishambulia, lakini haina mpango wa kuendeleza mashambulizi ikiwa Israel haitoshambulia.


Huu hapa ni muhtasari wa mambo yaliyotokea jana kuhusu mvutano wa nchi hizi mbili:


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian alisema shambulio la nchi yake ni sawa na "kutumia haki yake ya kujilinda" na Iran haitasita kulinda maslahi yake katika siku zijazo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alitoa wito kwa pande zote "kujizuia" na viongozi wengine kadhaa wa ulimwengu pia wametaka mvutano usikuzwe.

Ikulu ya Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron wameeleza shambulio la Iran halikufaulu.

Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani ni miongoni mwa nchi zilizowaita mabalozi wa Iran na kulaani huku zikiongeza shinikizo la kimataifa dhidi ya Tehran.

Msemaji wa masuala ya usalama wa taifa wa Ikulu ya Marekani, John Kirby alidai kiasi cha misaada inayoingia Gaza kimeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Lakini watu wengi wa Gaza bado wameyahama makazi yao kutokana na mapigano na kushindwa kurejea nyumbani, huku mashirika ya misaada yakionya juu ya baa la njaa

0 Comments:

Post a Comment