TBS Tatizo si 'Energy drinks" bali namna mnavyoitumia

 




"Spirits zote TBS tunazo viwango, energy drinks tunazo viwango, tatizo ambalo lipo wala siyo la ubora wala usalama wa hiyo bidhaa , nyie wanahabari mnaweza kuwa mashahidi, kwa wale tunaokunywa na kati yetu tupo,  kwamba unachukua chupa nzima ya Hennesy au unachukua chupa nzima ya Redbull ukikaa pale baa ile chupa inalazwa huwa haisimami wima,  halafu mtu anakunywa chupa nzima na bado akija rafiki yake anataka amwongezee,  matokeo yake  sasa unaifanya figo kuelemewa ukienda hospitali wanasema una tatizo la figo halafu kisingizio bidhaa ndizo zenye tatizo, yote yanasababishwa na matumizi mabaya ya bidhaa, kwa hiyo watanzania wengi tunatumia vibaya bidhaa hizo"- Lazaro Msasalaga 


"Hata energy drinks ukiziangalia zinadhibitiwa vizuri tu na kwenye maelekezo yake ukisoma vizuri imeandikwa unywe kiasi gani kwa siku lakini watu wanakunywa tu, wengine hata hawali yaani wanakunywa, na unajua kwa sababu ni energy drinks, huli chakula halafu unakunywa energy drinks maana yake unapata caffeine ambayo ndiyo inayokupa nguvu , kwenye energy drinks tunazungumzia caffeine (kilichomo) ambapo viwango vinasema isizidi 300, sasa kwa maana ya udhibiti inafanyika lakini kwa namna inavyotumika, mmiliki wa bidhaa anakwambia hii enery drink kwa siku labda utumie moja au mbili, hebu fikiria mtu anayefanya kazi nzito Dar es salaam na joto lilivyo anakunywa energy drinks ngapi kwa siku, kwa hiyo sisi tunachofahamu kwamba bidhaa hizi  na nyingine nyingi zinadhibitiwa ipasavyo ila kwa energy drinks na vinywaji vingine vigumu tunavitumia vibaya" - Lazaro Msasalaga 


Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga akizungumza na wanahabari Jumatatu Aprili 15, 2024 jijini Dar es Salaam wakati  TBS ikiwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio  kwa miaka ya hivi karibuni.

0 Comments:

Post a Comment