Padre Emmanuel Makolo wa Parokia ya Ndala Afariki Dunia

 


Emmanuel Makolo, aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Ndala katika Jimbo Katoliki la Shinyanga, amefariki dunia  Alhamisi, tarehe 25 Aprili 2024, majira ya saa tatu usiku, katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Kifo chake kimetangazwa na uongozi wa jimbo hilo. Padre Makolo alikuwa mtumishi mwaminifu wa kanisa na jamii yake, akihudumu kwa upendo na uaminifu mkubwa. 

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika kulingana na mila na desturi za kanisa na jamii.

Familia, marafiki, na waumini wote wanaomboleza kwa pamoja kumpoteza Padre Makolo, na kumwombea apumzike kwa amani.


0 Comments:

Post a Comment