Samia kushiriki Kumbukumbu ya Miaka 40 ya Kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine:
Kuenzi Mchango Wake Kwa Taifa
Ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 40 tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, imepangwa kufanyika Ijumaa, Aprili 12, 2024, katika Kijiji cha Enguik, Monduli Juu mkoani Arusha.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia, Lembris Marangushi Kipuyo, imethibitisha kuwa ibada hiyo itaanza saa 3:00 asubuhi na itaongozwa na viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Lengo kuu la ibada hiyo ni kuenzi na kukumbuka mchango mkubwa wa Hayati Sokoine katika maendeleo ya taifa.
Taasisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine imeanzishwa kwa lengo la kuendeleza kazi zake katika masuala ya elimu, kilimo, mazingira, vyanzo vya maji, na afya.
Hayati Sokoine, aliyefahamika kama mzalendo wa kweli, alijitolea kwa dhati katika utumishi wake kwa wananchi na alikuwa na hofu ya Mungu katika kutekeleza majukumu yake.
Alizaliwa Agosti 01, 1934, kijijini Enguik, Monduli Juu wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Tukio hili linatarajiwa kuwa fursa ya kuwakumbuka na kuenzi viongozi waliojitoa kwa dhati katika kuwatumikia wananchi na kuweka alama za kudumu katika historia ya taifa letu.
0 Comments:
Post a Comment