Ruge wa Chadema Ashinda Tuzo ya Ubunifu katika Kuwawezesha Wanawake
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa, Catherine Ruge, ameibuka mshindi wa tuzo ya Ubunifu katika Kuwawezesha Wanawake (Innovation in Women Empowerment).
Tuzo hizo, zilizojulikana kama EmpowerHer Excelency Award, zinatambua juhudi za wanawake na taasisi katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kijamii.
Hafla hiyo ya kipekee ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.
Catherine alikiri kwamba mafanikio hayo ni ya pamoja na wanawake wengine wanaopigania haki zao na usawa katika jamii. Tuzo hii inaashiria hatua muhimu katika kujenga jamii yenye usawa na fursa kwa kila mmoja.

0 Comments:
Post a Comment