Mwandishi wa Habari wa Ahukumiwa Miezi Sita Jela kwa Kueneza Habari za Uongo

 Mwandishi wa Habari wa Ahukumiwa Miaka Sita Jela kwa Kueneza Habari za Uongo



Mahakama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilimhukumu mwandishi wa habari wa Congo, Stanis Bujakera, kifungo cha miezi sita jela siku ya Jumatatu. 

Hii ni baada ya kumpata na hatia ya kueneza habari za uongo pamoja na mashtaka mengine. 

Bujakera, ambaye anafanya kazi katika vyombo vya habari vya kimataifa kama vile Jeune Afrique na Reuters, amekuwa akishikiliwa tangu Septemba mwaka jana. 

Wakili wake, Jean-Marie Kabengela, alithibitisha hukumu hiyo na kueleza kuwa Bujakera anatarajiwa kuachiliwa baada ya kutumikia muda huo. 

Hata hivyo, timu ya mawakili itarejea mahakamani kupata nakala ya uamuzi na kulipa faini ili aachiliwe.

Bujakera alikamatwa kwa tuhuma za kueneza habari za uongo kuhusu mauaji ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani, kama ilivyochapishwa na Jeune Afrique. 

Awali, mwendesha mashtaka alitaka ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela. 

Hata hivyo, mashirika ya haki za binadamu, pamoja na Reporters Without Borders na Amnesty International, yalaani kuzuiliwa kwake na kuitaja kama shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari. Reuters nayo imetoa wito wa kuachiliwa kwake.

0 Comments:

Post a Comment