EU Yachunguza Makampuni ya Teknolojia kwa Ukiukaji wa Sheria za Masoko ya Kidijitali


EU Yachunguza Makampuni ya Teknolojia kwa Ukiukaji wa Sheria za Masoko ya Kidijitali



Umoja wa Ulaya (EU) umezindua uchunguzi dhidi ya makampuni makubwa zaidi ya teknolojia duniani, ikiwa ni pamoja na Alphabet, kwa madai ya mbinu za kibiashara zisizo halali na ushindani.

 

Uchunguzi huo unalenga kubaini ikiwa kampuni hizo zimekiuka Sheria ya Masoko ya Kidijitali iliyowekwa mwaka wa 2022.

 

Kampuni hizo zinaweza kukabiliwa na faini kubwa hadi 10% ya mauzo yao ya kila mwaka ikiwa watapatikana na hatia.

 

Hatua hii inakuja baada ya EU kutoza Apple faini ya euro bilioni 1.8 kwa ukiukaji wa sheria za ushindani kuhusu utiririshaji wa muziki.

 

Wakati huo huo, Marekani pia imeshutumu Apple kwa kuhodhi soko la simu za kisasa.

 

Kampuni zinazochunguzwa zimeahidi kushirikiana kikamilifu na uchunguzi huo na kudai kuwa zinazingatia sheria muhimu za EU, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa faragha na usalama wa watumiaji wa EU.

Chanzo BBC







0 Comments:

Post a Comment