Waziri Mpya wa Ulinzi wa Liberia Ajiuzulu Baada ya Maandamano

Waziri Mpya wa Ulinzi wa Liberia Ajiuzulu Baada ya Maandamano


Waziri mpya wa ulinzi wa Liberia, Prince .C. Johnson, amejiuzulu kutoka kwenye wadhifa wake siku 10 tu baada ya kuteuliwa, kufuatia maandamano yaliyofanywa na wake wa wanajeshi wa nchi hiyo.


Macho yote yalikuwa yameelekezwa kwa Johnson alipoteuliwa kushika wadhifa huo, lakini ghafla ameamua kujiuzulu, jambo ambalo limezua maswali mengi miongoni mwa wananchi wa Liberia. Uamuzi wake wa kujiondoa umeonekana kama mshangao mkubwa, hasa kwa kuzingatia muda mfupi tangu ateuliwe.

Rais Joseph Boakai 


Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais imeeleza kuwa Rais Joseph Boakai mepokea na kukubali barua ya kujiuzulu kwa waziri huyo. Katika barua yake, Johnson ameeleza kwamba machafuko ya kisiasa na ya kiraia yaliyosababisha maandamano yamekuwa sababu ya kujiuzulu kwake, akisema amefanya hivyo ili "kulinda amani na usalama wa nchi."


Maandamano yaliyofanywa na wake wa wanajeshi yalikuwa na lengo la kushinikiza serikali kuboresha masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara ya wanajeshi na kuboresha huduma za kijamii. Wanawake hao walitia fora kwa kuweka vizuizi barabarani, ikiwa ni pamoja na karibu na mji mkuu Monrovia, huku wakimtaka rais Boakai kuchukua hatua za haraka kutatua madai yao.


Rais Boakai, ambaye amekabiliana na maandamano haya kama changamoto ya kwanza tangu aingie madarakani, amewataka watu kuwa watulivu, akiahidi kuwa serikali yake itatatua matatizo yao. Hata hivyo, hatua ya Johnson kujiuzulu ni ishara kwamba shinikizo la umma linaweza kuleta mabadiliko katika utawala wa nchi hiyo.

0 Comments:

Post a Comment