PROF NDAKIDEMI AJENGA OFISI YA TARAFA

 PROF NDAKIDEMI AJENGA OFISI YA TARAFA


Na Gift Mongi,Moshi


Ni katika kuendelea kuleta huduma karibu na wananchi Kwa kuhakikisha kuwa ofisi za viongozi wa tarafa zinakuwa karibu na wananchi tofauti na miaka ya nyuma.



Katika kuhakikisha hayo yote yamefanyika kisawasawa kama ilivyokuwa katika ilani ya uchaguzi wa CCM(2020-2025) tayari ujenzi wa ujenzi wa ofisi ya Tarafa ya Hai Mashariki umekamilika katika Kata ya Kimochi.


Kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo ni jitihada kubwa zilizoelezwa kuwa ni msukumo kutoka kwa mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi.


'Niliahidi na nashukuru nimeweza kutekeleza ila pia sio jitihada zangu pekee ila pia lazima tuwashukuru pia madiwani kwa jitihada zao'anaeleza Prof Ndakidemi


Diwani wa Kibosho Kirima Inyasi Mushi amesema kukamilika kwa ofisi hizo kutaenda kuleta ma ndeleo na huduma karibu Kwa wananchi


'Tujipongeze kwa hatua hii muhimu tulipofikia hakika huu ndio uongozi wenye kuacha alama kwa wananchi wetu'anasema


Wilhad Kitally ni diwani wa Uru Kusini ambapo alisema kukamilika kwa ofisi hiyo ni utekelezaji wa ilani ambayo iliahidiwa na mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi katika kampeni zake.


'Amekuwa ni mbunge wa vitendo kwani kinachofanywa sasa ni kile ambacho aliahidi nafikiri tuendelee kumuunga mkono kama madiwani ili tusogeze maendeleo'Amesema



0 Comments:

Post a Comment