Vilio majonzi vyatawala Arusha wakiaga miili ya walikufa ajali ya Ngaramtoni

 Vilio majonzi vyatawala Arusha wakiaga miili ya walikufa ajali ya Ngaramtoni



Leo, maelfu ya wananchi wamekusanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa Arusha kutoa heshima za mwisho kwa marehemu wa ajali mbaya iliyohusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la Ngaramtoni. 



Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Pindi Chana, ameongoza shughuli hiyo ya kuguswa moyo, akitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.



Kati ya watu 25 waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo, miili ya 11 imeagwa leo, huku familia zikiendelea kuchukua miili ya wengine 14. Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali wametoa maneno ya faraja kwa familia za waathirika, wakiongozwa na Dkt. Stanlet Hotay kwa upande wa Kikristo na Sheikh Hussein Said kwa upande wa Kiislam.



Balozi Dkt. Pindi Chana amewasilisha salamu za pole za serikali, huku Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella akiwasilisha maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kushiriki kikamilifu katika mazishi kama njia ya kufariji wafiwa.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Ole Sabaya, amewasilisha salamu za Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi. 



Aidha, Kaimu Balozi wa Kenya nchini, Nancy Sifa, ametoa salamu za pole kutoka serikali ya Kenya kufuatia raia wake waliopoteza maisha katika ajali hiyo.


Mazishi yanaendelea kufanyika huku taifa likiendelea kuomboleza na kusali kwa familia zilizoathirika katika janga hili la ghafla.








0 Comments:

Post a Comment